Monday, March 25, 2013

VIDEO: KAJALA ALIPOINGIA URAIANI

BREAKING NEWS!!! KAJALA AINGIA URAIANI KUPITIA MIKONO YA WEMA SEPETU



Msanii wa Bongo Movie Kajala Masanja ambae alikuwa anakabiliwa na kesi ya jinai leo kesi hiyo ilisomwa na kutolewa hukumu mbele ya hakimu mkazi kunako mahakama ya kisutu jiji Dar es Salaam. Hakimu Sudi Fimbo alisoma hukumu hiyo ya kumtaka Kajala kwenda gerezani kwa kifungo cha miaka mitano au faini ya shilingi za kitanzania milioni 13. Inaaminika kuwa Wema Sepetu ndio aliojitolea kiasi hicho cha hela na kusababisha Kajala kuingia mtaani. Big Up to Wema Sepetu.

Sunday, March 24, 2013

MADEE AMPA SHAVU DIAMOND KWENYE VIDEO YA NGOMA YAKE MPYA "POMBE YANGU"





Baadhi ya picha zikionesha sehemu ya maandalizi ya kioo kipya cha super raper kutoka mitaa ya Manzese jijini Da er Salaam. Rais Huyo wa Manzese kama anavyotambulika pia amempa shavu rais wa wasafi Diamond Platnumz kwenye kideo hicho. 
Hata hivyo mmoja wa wadau wa kundi la TipTop ambalo ndilo kundi linalomtambulisha Madee, bwana Hamisi Talle "Bab Talle" amekaririwa akisema kuwa video hiyo itatoka hivi karibuni na itakuwa video hatari kwa ubora wake. "kaka tusiongee mengi wewe subiri utaona mwenyewe kazi ikitoka" alisema Talle hivi juzi kati kwa njia ya simu alipoongea na mwakilishi wa blog hii.



Thursday, March 21, 2013

"NEEMA WA MITEGO" NDIO JINA LA NGOMA MPYA YA NIKI MBISHI


Mbishi na Pozi la nguvu

Msanii wa muziki wa kufokafoka (HipHop) pande za Bongo mwenye jina kubwa kutokana na ubishi wake katika fani "Niki Mbishi" amefunguka na kusema ngoma yake mpya inatoka hivi karibuni ambayo itakwenda kwa jina la Ney wa mitego. Mbishi alifunguka na kusema kuwa ngoma hyo haina mahusiano yoyote na msanii Ney Wamitego na wala hajamzungumzia bali inamuhusu mwanadada Neema wa mitego ambaye kifupi chake ni Ney.

Mbishi amewataka mashabiki wake na mashabiki wa muziki kukaa mkao wakula na kusikiliya maisha halafu wao ndo watakuwa waamuzi. Aliendelea kusisitiza kuwa hiyo ngoma inamuhusu mwanadada Neema wa Mitego.

RICH ONE AINGIA TENA KWENYE KASHFA YA UTAPELI



Msanii wa longtime kwenye game ya bongo fleva kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam "Rich One" ambaye alikuwa na tuhuma za utapeli kwa kutumia jina la msanii Ally Kiba miezi kadhaa iliyopita. Hivi juzi amekumbwa na skendo nyingine ya utapeli wa kutumia jina la msanii mwingine wa bongo fleva "Stamina"

Inasemekana kuwa Rich one amekuwa akijifanya kuwa yeye ni Meneja wa stamina huku akiwasiliana na waandaji matamasha na kuwaahidi kuwaletea msanii huyo kwenye matamasha. Huku akiwa amemtengeneza mtu asiyejulikana na kumtambulisha kuwa ndo msanii Stamina kwa njia ya simu.



Tuesday, March 5, 2013

ONA MWENYEWE JINSI WADADA WALIVYOPENDEZA AFTER WORK PARTY







































AFTER WORK PARTY ILIKUWA NOMA!!!




Dj Rama na Dj Lady Kiarie



Just Chillin men!!!!!!



Sanaa tu!!!!!



Masharoooo!!!!!



Burudani mwanzo mwisho



Dj Tindo & Dj Max




Promota Malumbo




Mtu mzima Tege ndani ya nyumba






Full kujiachia



Papaaaa!!!



kukatika nayo.......



Ni kama alikuwa anasema "Dj Max is Number 1 "



Warembo!!!!!!



Utamu wa ngoma



Hapo sasa!!!!






Mzee wa Chabo



One Love


Sunday, March 3, 2013

MCHUMIA TUMBO AMCHAKAZA MARWA




Bondia anaekuja kwa kasi sana katika fani ya masumbwi kutoka mitaa ya Temeke jijini Dar es Salaam anaejulikana kwa jina maarufu la Mchumia tumbo, usiku wa jana amemtoa kijasho na kumpa kichapo mkongwe Josseph Marwa.