Friday, February 15, 2013

MWANARIADHA WA AFRIKA KUSINI (OSCAR PISTORIUS) AMUUA MPENZI WAKE SIKU YA VALENTINEPolisi nchini Afrika kusini wamethibitisha kuupata mwili mwanamitindo Reeva Steenkamp ambae alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanariadha Oscar Pistorius. Mwili huo ambao ulikuwa umbeshambuliwa kwa kupigwa risasi nne sehemu tofauti ulikutwa nyumbani kwa mwanariadha huyo siku ya wapendanao, ambaopo ilithibitika kuwa Oscar ndiye mtuhumiwa namba moja kwa kuwa hakukuwa na mtu yoyote ndani ya nyumba hiyo zaidi ya wawili hao.

Akitoa maelezo yake mbele ya maafisa wa polisi Oscar alisema kuwa siku hiyo alikuwa nyumbani peke yake huku akiwa hana matarajio ya kupata mgeni, laini mpenzi wake huyo alikuja kumtembelea kwa kushtukiza "suprise" lakini yeye hakugundua na kufikiria kuwa labda kavamiwa na majambazi. Wakati akijaribu kujihami akaamua kurusha risasi na baada ya kumshambulia mtu huyo ambae alifikiri kuwa ni jambazi ndipo baadae akagundua kuwa amemuua mpenzi wake. Hata hivyo maafisa wa Polisi hawajatoshelezwa na maelezo hayo yaliyotolewa na Oscar, hivyo uchunguzi bado unaendelea.


Oscar alipokuwa akichuliwa na polisi nyumbyni kwake

No comments:

Post a Comment