Sunday, April 21, 2013

OMMY DIMPOZ ATUA OSLO READY FOR THE SHOW!!!
Camera ya Dj Max ilimnasa Dimpoz akiwa kwenye poz na mwenyeji wake Dj Pred wa Norway:

Akitiririka wakati wa mahojiano nae, Dimpoz alifunguka kuwa kuna uwezekano wa kuongeza siku za ziara yake kutokana na maombi ya mashabiki na show kuongezeka. kwani katika ratiba yake hakukuwa na nchi kama Ujerumani lakini kutokana na maombi ya mashabiki Dimpoz anafikiria kubwaga show la nguvu ndani ya Bayern siku za hivi karibuni.Mapoz yanaendelea:

Pia alisisitiza kuwa ana vitu muhimu vya kuwahi nyumbani kwahiyo hatoongeza muda mrefu sana, ikiwemo na kuhudhuria tuzo za muziki za Killi. "Naenda kuwafunika mwana, si unajua kuna tuzo zangu kadhaa na lazima nivunje record mwaka huu" alisema Dimpoz huku akitabasamu kuashiria kuwa anajiamini lakini katika hali ya utani.


No comments:

Post a Comment