Monday, October 29, 2012

WIMBO MPYA WA DIAMOND "nataka kulewa" BONYEZA HAPA KUSIKILIZA

HONGERA J4 KWA KUCHUKUA JIKO



J4 akiwa na mwandani wake baada ya kufunga pingu za maisha katika pozi lenye tabasamu la nguvu kwa furaha


Chanda chema huvishwa pete, kwa uzima na ugonjwa mpaka kifo



Wadau wa Augsburg nao waliwakilisha, kutoka kulia Malumbo S Malumbo (mambo bado Sounds), Othman Babu (Black Mamba) bwana harusi na bibi harusi.


Monday, October 22, 2012

CHEGE CHIGUNDA AKANUSHA KUMTIA MIMBA MKE WA MTU



Msanii mwenye jina kubwa ndani ya bongo kutoka mitaa ya Temeke jijini Dar es Salaam leo alifunguka alipokuwa akipiga "story" na kipindi cha XXL cha clouds fm. Chege alikanusha vikali tuhuma au uzushi huo uliokuwa umezagaa kila kona baada ya kubainika kuwa mtu huyo hakuwa na ushahidi sababu ambayo imempelekea Chege kusema kuwa atachukua hatua na taratibu za kisheria dhidi ya mtu huyo


Friday, October 19, 2012

OGOPA DEEJAYZ NDIO WATAKAO HUSIKA KATIKA KUANDAA VIDEO YA WIMBO MPYA WA TUNDA MAN



Msanii kutoka kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake maeneo ya Magomeni jiji Dar es Salaam "Tunda Man" leo aliamua kufunguka kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa "Face Book". Tunda aliamua kuwatoa hofu mashabiki wa masongi yake yake kwa kuandika kuwa ngoma mpya tayari imekamilika kwa upande wa sauti na kinachofuata ni video ambayo itafanywa nchini kenya na wakali wa siku wa muziki wa Afrika Mashariki "Ogopa Deejayz". Alimalizia kwa kusema kaeni mkao wa kula, mambo matam na mazuri yanakuja.