Friday, October 19, 2012

OGOPA DEEJAYZ NDIO WATAKAO HUSIKA KATIKA KUANDAA VIDEO YA WIMBO MPYA WA TUNDA MANMsanii kutoka kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake maeneo ya Magomeni jiji Dar es Salaam "Tunda Man" leo aliamua kufunguka kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa "Face Book". Tunda aliamua kuwatoa hofu mashabiki wa masongi yake yake kwa kuandika kuwa ngoma mpya tayari imekamilika kwa upande wa sauti na kinachofuata ni video ambayo itafanywa nchini kenya na wakali wa siku wa muziki wa Afrika Mashariki "Ogopa Deejayz". Alimalizia kwa kusema kaeni mkao wa kula, mambo matam na mazuri yanakuja.

No comments:

Post a Comment