Thursday, September 26, 2013
MATOKEO YA ROUND YA PILI YA DFB-POKAL, BAYERN ASHINDA KAMA KAWA
Katika round ya pili ya DFB-Pokal (kombe la Ujerumani) hazijtakoea maajabu. Timu zote za Erste Bundesliga (daraja la kwanza) zilizocheza na timu za daraja la chini zilishinda. Katika mechi zote mbinu ni kwamba anayefungwa anatoka moja kwa moja kwa hiyo mechi zote ni kama fainali.Dortmund na Hoffenheim walipata taabu kidogo, imebidi waongezewe muda ili wachukue ushindi.
Wednesday, September 18, 2013
BAYERN WALIPOFUNGA ZSKA MOSKAU KATIKA MECHI YAO YA KWANZA YA CHAMPIONS LEAGUE MSIMU HUU
David Alaba akishangilia kufunga goli la kwanza kwa timu ya Nyota ya Kusini FC Bayern München.
Kocha mpya Pep Guardiola akiwaelekeza wachezaji wake jinsi ya kucheza.
Matokeo:
FC BAYERN MÜNCHEN 3:0 ZSKA MOSKAU
Sunday, May 26, 2013
MARIO MANDZUKIC, AWEKA HISTORIA KUWA RAIA WA KWANZA WA KROATIA KUFUNGA GOLI KWENYE FAINALI ZA CHAMPIONS LEAGUE
Ni mzaliwa wa Slavonski Brod nchini Kroatia ambaye ana umri wa miaka 27, kwa maana ya kuwa alizaliwa mwaka 1986 mwezi mei tarehe 21. Nyota yake imeanza kumeremeta zaidi msimu huu wa Bundesliga alipojiunga na FC Bayern akiwa anatokea Wolfsburg.Alizidi kujiongezea umaarufu siku hadi siku kwa umahiri wake wa kufunga angalau goli moja katika kila mechi aliyocheza na jana ameandika historia kuwa raia wakwanza kutoka Kroatia kupachika goli kwenye fainali za mabingwa wa Ulaya.
Monday, May 20, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)



