Sunday, May 26, 2013

MARIO MANDZUKIC, AWEKA HISTORIA KUWA RAIA WA KWANZA WA KROATIA KUFUNGA GOLI KWENYE FAINALI ZA CHAMPIONS LEAGUENi mzaliwa wa Slavonski Brod nchini Kroatia ambaye ana umri wa miaka 27, kwa maana ya kuwa alizaliwa mwaka 1986 mwezi mei tarehe 21. Nyota yake imeanza kumeremeta zaidi msimu huu wa Bundesliga alipojiunga na FC Bayern akiwa anatokea Wolfsburg.Alizidi kujiongezea umaarufu siku hadi siku kwa umahiri wake wa kufunga angalau goli moja katika kila mechi aliyocheza na jana ameandika historia kuwa raia wakwanza kutoka Kroatia kupachika goli kwenye fainali za mabingwa wa Ulaya.

No comments:

Post a Comment