Saturday, June 16, 2012

BAADA YA KIMYA CHA MUDA MFUPI DJ RAMA AFUNGUKA


LEO MAMBO DOLE TUPU


Unapoizungumzia safu ya ma Dj machachari nchini ujerumani bila shaka hautamaliza kauli yako bila ya kutaja jina Rama (The best Dj), espescially when you talk about Munich na Bayern kwa ujumla.

Baada ya kuwa kimya kwa muda kidogo, leo amefunguka na kutamka waziwazi kwa mashabiki zake kuwa amewaandalia ngoma za kufa mtu usiku wa leo. Ameweka wazi kuwa watarajie burudani ya aina yake kutoka kwake amerudi na masongi mapya kibao ambayo hayana hata idadi.

Dj Rama anatarajiwa kufanya makamuzi leo usiku katika jiji la Nurberg pembeni kidogo ya mji wa Munich katika jimbo la Bayern. Ambapo Dj Max Entertainments imeandaa sherehe za Madaraka Day. Shuguli hiyo itafanyika pale maeneo ya Club Festac 77, Zufuhrstr 20. Kwa dada Jeniffer.

Bila kusahau utambulisho wa Dj Lady kiarie na Dj Mukada huku Mdogo wao wa mwisho Dj Max nikiwasindikiza. Burudani hizi zote utazipata kwa dau la kiingilio cha 5€ pekee.

KILA MMOJA AMEKARIBISHWA

No comments:

Post a Comment