Wednesday, June 27, 2012

BAADA YA ZAIDI YA MIAKA 25 MCHEZAJI MKONGWE KASSIM MANARA(MJOMBA) ADEKA KWA MAMA YAKE




Kassim Manara (Mjomba) akideka kwa mama yake mzazi baada ya kutokuonana kwa zaidi ya miaka 25.

 Manara ndio mchezaji pekee wa Tanzania aliewahi kuchezea timu kubwa zaidi duniani. Katika maisha yake amewahi kuchezea  timu ya Borussia Dortmund ya ujerumani.




Mjomba Manara akiwa na wajukuu na vitukuu ambao walimtia machoni kwa mara ya kwanza tangu kuzaliwa kwao.



Mjomba Kassim Manara akiwa na dada zake pamoja na mama mzazi



Manara akiwa na vijana wake wa mtaani maeneo ya Temeke jijini Dar 

Kwa niaba ya Dj Max Entertainments and the crew tunamuombea maisha marefu na yenye afya bw. Kassim Manara almaarufu kama Mjomba. Pia mungu amzidishie moyo wa imani alionao.

Kwa kifupi tu ni kwamba jina la mjomba amepewa na vijana wa kitanzania anaoishi nao majuu kutokana na misaada na michango yake mbalimbali ya hali na mali. Pia ukarimu wake na urafiki, heshima aliyonayo kwa wakubwa na wadogo na ukaribu alionao pia imechangia



No comments:

Post a Comment