DOGO JANJA APIGWA CHINI TIP TOP
Msanii kinda kwenye kundi la Tip Top lenye maskani yake mitaa ya Manzese jijini Dar es salaam, Abdul Abubakar Chende "Dogo janja". Amejikuta akifungashiwa virago vyake na kutengwa na kundi hilo kutokana na tabia za utovu wa nidhamu na kuendekeza starehe, kikubwa akiwa ni tabia yake ya kukataa kwenda shule.
Hayo yalielezwa na kiongozi wa kundi hilo bwana Hamad Ally "Madee" alipopiga stori na teentz. Kwa niaba ya wapenda maendeleo nampa shavu madee kwa kujaribu kumuendeleza dogo huyo kielimu kwa kumsihi aende shule mara kwa mara lakini bahati mbaya bwana mdogo kalewa umaarufu.
No comments:
Post a Comment