Thursday, December 20, 2012

BREAKING NEWS!!!! Q CHIEF ATANGAZA RASMI KUACHANA NA MADAWA YA KULEVYA NA KUWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE NA KUTOA NGOMA MPYA

Kama wewe ni shabiki wa muziki wa kizazi kipya ndani ya Afrika Mashariki bila shaka jina Q-chillah wala haliwezi kuwa geni masikioni mwako. Mwanamuziki huyu kutoka jiji Da es Salaam Tanzania, leo amekiri ndani ya kipindi cha xxl cha Clouds Radio alipokuwa akipiga stori na Adam Mchomvu "BABA JONII"  kuwa alikuwa akitumia dawa za kulevya kwa takriban miaka miwili na kwa sasa ameacha kutumia kwa zaidi ya miezi saba.

Ingawa hakuweka wazi ni dawa zipi alikuwa akizitumia na kwa njia zipi lakini alisema kwa sauti ya kusikitisha kuwa "kaka we acha tu nimepitia mengi". Pia alikuwa akikataa kujibu baadhi ya maswali kwa kile alichokieleza kuwa akiongelea swala hilo linamletea kumbukumbu mbaya ambazo hapendi kuzikumbuka kwa sasa.

Pia alichukua nafasi hiyo kuwaomba msamaha mashabiki wake, ndugu jamaa na marafiki endapo alikuwa amewakosea kwa tabia hiyo aliyokuwa nayo kipindi hicho. Alisisitiza kuwa amefanya maamuzi ya kuacha uteja kwa ajili ya watoto wake na wazazi wake pia, kwani anaamini kuwa aliwaumiza sana.

HONGERA SANA CHILLAH

No comments:

Post a Comment