Sunday, July 1, 2012
Wednesday, June 27, 2012
BAADA YA ZAIDI YA MIAKA 25 MCHEZAJI MKONGWE KASSIM MANARA(MJOMBA) ADEKA KWA MAMA YAKE
Kassim Manara (Mjomba) akideka kwa mama yake mzazi baada ya kutokuonana kwa zaidi ya miaka 25.
Manara ndio mchezaji pekee wa Tanzania aliewahi kuchezea timu kubwa zaidi duniani. Katika maisha yake amewahi kuchezea timu ya Borussia Dortmund ya ujerumani.
Mjomba Manara akiwa na wajukuu na vitukuu ambao walimtia machoni kwa mara ya kwanza tangu kuzaliwa kwao.
Mjomba Kassim Manara akiwa na dada zake pamoja na mama mzazi
Manara akiwa na vijana wake wa mtaani maeneo ya Temeke jijini Dar
Kwa niaba ya Dj Max Entertainments and the crew tunamuombea maisha marefu na yenye afya bw. Kassim Manara almaarufu kama Mjomba. Pia mungu amzidishie moyo wa imani alionao.
Kwa kifupi tu ni kwamba jina la mjomba amepewa na vijana wa kitanzania anaoishi nao majuu kutokana na misaada na michango yake mbalimbali ya hali na mali. Pia ukarimu wake na urafiki, heshima aliyonayo kwa wakubwa na wadogo na ukaribu alionao pia imechangia
Tuesday, June 19, 2012
MADARAKA DAY NÜRNBERG ILIBAMBA MBAYA
Baadhi ya watu waliokuwa ukumbini wakibanjuka
Dj Rama na Dj Mukada wakiongoza Mashambulizi
Masharobaro wa kipopo (mashemeji) nao walikuwepo
Wazee wa vitambi nao ndani
Warembo full kujiachia
Pozi la usingizi
Saturday, June 16, 2012
BAADA YA KIMYA CHA MUDA MFUPI DJ RAMA AFUNGUKA
LEO MAMBO DOLE TUPU
Unapoizungumzia safu ya ma Dj machachari nchini ujerumani bila shaka hautamaliza kauli yako bila ya kutaja jina Rama (The best Dj), espescially when you talk about Munich na Bayern kwa ujumla.
Baada ya kuwa kimya kwa muda kidogo, leo amefunguka na kutamka waziwazi kwa mashabiki zake kuwa amewaandalia ngoma za kufa mtu usiku wa leo. Ameweka wazi kuwa watarajie burudani ya aina yake kutoka kwake amerudi na masongi mapya kibao ambayo hayana hata idadi.
Dj Rama anatarajiwa kufanya makamuzi leo usiku katika jiji la Nurberg pembeni kidogo ya mji wa Munich katika jimbo la Bayern. Ambapo Dj Max Entertainments imeandaa sherehe za Madaraka Day. Shuguli hiyo itafanyika pale maeneo ya Club Festac 77, Zufuhrstr 20. Kwa dada Jeniffer.
Bila kusahau utambulisho wa Dj Lady kiarie na Dj Mukada huku Mdogo wao wa mwisho Dj Max nikiwasindikiza. Burudani hizi zote utazipata kwa dau la kiingilio cha 5€ pekee.
KILA MMOJA AMEKARIBISHWA
Friday, June 15, 2012
Wednesday, June 13, 2012
DOGO JANJA APIGWA CHINI TIP TOP
Msanii kinda kwenye kundi la Tip Top lenye maskani yake mitaa ya Manzese jijini Dar es salaam, Abdul Abubakar Chende "Dogo janja". Amejikuta akifungashiwa virago vyake na kutengwa na kundi hilo kutokana na tabia za utovu wa nidhamu na kuendekeza starehe, kikubwa akiwa ni tabia yake ya kukataa kwenda shule.
Hayo yalielezwa na kiongozi wa kundi hilo bwana Hamad Ally "Madee" alipopiga stori na teentz. Kwa niaba ya wapenda maendeleo nampa shavu madee kwa kujaribu kumuendeleza dogo huyo kielimu kwa kumsihi aende shule mara kwa mara lakini bahati mbaya bwana mdogo kalewa umaarufu.
Tuesday, June 12, 2012
KWANI LULU ANAMIAKA MINGAPI???? UMRI WAKE SAHIHI NI UPI???
Mahakama ya Tanzania leo kwa Makusudi wameamua kumpunguzia miaka
Subscribe to:
Posts (Atom)






