Sunday, September 9, 2012

JUMA NATURE BADO NI NOMA!!!! AFUNIKA FIESTA TABORA KINOMA NOMA



Anaitwa Juma Kassim Kiroboto, mtoto wa Temeke jijini Dar. Ingawa wengi hupenda kumuita Juma nature au Sir nature. Pamoja na kuwa hajadondosha songi jipya kwa muda mrefu kidogo lakini pindi anapopanda jukwaani huwatia uchizi mashabiki wake wa masongi yake ya kitambo. Bado kuna watu wanajiuliza je? anatumia kizizi?

"Huyu jamaa hajatoa wimbo mpya lakini alipopanda tu watu wote walichanganyikiwa kwa furaha, sijui ana kizizi" moja ya mashabiki alisikika akisema baada ya tamasha la Fiesta lililofanyika mjini Tabora ambalo liliandaliwa na wakali wa burudani nchini Tanzania Clouds radio (the people station)

Saturday, September 8, 2012

JULIA NJOROGE FROM KENYA IS MISS EAST AFRIKA BELGIU 2012



Kwa niaba ya The Dj Max Entertainments and the crew, tunakupa hongera sana dada yetu kwa kushinda taji la Miss East Africa Belgium. Hongera pia kwa waandaji bila za kumsahau Azam, Kitokololo na the big bosss Denis Ruba

Wednesday, September 5, 2012

EAST vs WEST AFRICA PARTY IN MUNICH ILIKUWA NOMAA!!!!!


Super Dj Rama akifanya makamuzi



Bobby St akiwarusha mashabiki


Wadada warembooo!!!!!!!!!



Dj Lady Kiarie..... One Love!!!!



Cute girls


Just chilling and Enjoying



Mashabiki wakiburudika na kuburudishwa na Bobby st



Doctor Kingo in the house!!!!!!!  kaka rudi kazini wagonjwa watakufa



Hapa nimejichanganya na wenye Munich yao




NYOMI ZAIDI YA LILE!!!!!



HAPPY BIRTHDAY MATHIAS SAMMER (ZUM GERBUSTAG VIEL GLÜCK)




Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya ujerumani na ambae pia aliwahi kuichezea Dortmund, lakini kwa sasa ni kiongozi katika bodi ya michezo kwenye chama kubwa FC BAYERN MÜNCHEN. Herr Mathias Sammer leo amezaliwa na kwa pamoja tunasema "Zum Geburtag viel Glück "

Tuesday, September 4, 2012

MWANAKIJIJI ACHANGANYIKIWA KWA FURAHA YA KUKUTANA NA SHAFFIH DAUDA, MBWIGA WA MBWIGUKE (MZARAMU HALISI) NA BONGE

BI KIDUDE HAJAFAAAA!!!!! WACHENI KUMZUSHIA




Msanii maarufu na mzee kuliko wote Afrika mashariki, ambae ni mzaliwa wa Zanzibar katika Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TANZANIA). Fatma bint Baraka maarufu kama bi Kidude alizushiwa kuwa amefariki mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Taarifa za sahihi kutoka kwa wajukuu zake zinasema kuwa bibi bado yuhai  na kwa uwezo wa mungu ataishi maisha marefu zaidi japokuwa kwa sasa afya yake si nzuri kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambayo hawakuyataja. "Maradhi ni kitu cha kawaida na kila binaadamu huugua, ni kweli bibi anaumwa lakini hajafa na tunamuombea kwa mungu apate afueni" hayo yalisemwa na mjukuu wake ambaye pia ni msanii wa miondoko ya mduara kutoka visiwani nilipoongea nae kwa njia ya simu, lakini aliomba jina lake lisiandikwe hapa, nami nafanya hivyo kwa kumuheshimu na kuheshimu mawazo yake.