Sunday, September 9, 2012

JUMA NATURE BADO NI NOMA!!!! AFUNIKA FIESTA TABORA KINOMA NOMA



Anaitwa Juma Kassim Kiroboto, mtoto wa Temeke jijini Dar. Ingawa wengi hupenda kumuita Juma nature au Sir nature. Pamoja na kuwa hajadondosha songi jipya kwa muda mrefu kidogo lakini pindi anapopanda jukwaani huwatia uchizi mashabiki wake wa masongi yake ya kitambo. Bado kuna watu wanajiuliza je? anatumia kizizi?

"Huyu jamaa hajatoa wimbo mpya lakini alipopanda tu watu wote walichanganyikiwa kwa furaha, sijui ana kizizi" moja ya mashabiki alisikika akisema baada ya tamasha la Fiesta lililofanyika mjini Tabora ambalo liliandaliwa na wakali wa burudani nchini Tanzania Clouds radio (the people station)

No comments:

Post a Comment