Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya ujerumani na ambae pia aliwahi kuichezea Dortmund, lakini kwa sasa ni kiongozi katika bodi ya michezo kwenye chama kubwa FC BAYERN MÜNCHEN. Herr Mathias Sammer leo amezaliwa na kwa pamoja tunasema "Zum Geburtag viel Glück "
Wednesday, September 5, 2012
Tuesday, September 4, 2012
BI KIDUDE HAJAFAAAA!!!!! WACHENI KUMZUSHIA
Msanii maarufu na mzee kuliko wote Afrika mashariki, ambae ni mzaliwa wa Zanzibar katika Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TANZANIA). Fatma bint Baraka maarufu kama bi Kidude alizushiwa kuwa amefariki mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Taarifa za sahihi kutoka kwa wajukuu zake zinasema kuwa bibi bado yuhai na kwa uwezo wa mungu ataishi maisha marefu zaidi japokuwa kwa sasa afya yake si nzuri kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambayo hawakuyataja. "Maradhi ni kitu cha kawaida na kila binaadamu huugua, ni kweli bibi anaumwa lakini hajafa na tunamuombea kwa mungu apate afueni" hayo yalisemwa na mjukuu wake ambaye pia ni msanii wa miondoko ya mduara kutoka visiwani nilipoongea nae kwa njia ya simu, lakini aliomba jina lake lisiandikwe hapa, nami nafanya hivyo kwa kumuheshimu na kuheshimu mawazo yake.
Wednesday, August 29, 2012
Tuesday, August 28, 2012
Friday, August 24, 2012
DORTMUND WAANZA VIZURI KUTETEA UBINGWA WAO WA BUNDESLIGA
Picha ikionyesha shamrashamra zilivyotawala mjini Dortmund wakati wa mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya mpira wa miguu Ujerumani (Bundesliga), ambaopo mabingwa watetezi Borussia Dortmund waliwapa kichapo maridadi Werder Bremen cha Magoli mawili kwa moja.
Subscribe to:
Posts (Atom)



