Thursday, January 31, 2013

FILAMU YA MWISHO ALIYOCHEZA SHARO MILLIONEA KUWA MITAANI KESHO



Hussein "Sharo Milionea" enzi za uhai wake

Taarifa za kuaminika kutoka kwa familia ya "King Majuto" pamoja na Sharo zimetufikia hivi punde kuthibitisha kuwa ile filamu ya vichekesho aliyocheza Sharo siku chache kabla ya kukumbwa na umauti ambayo inajulikana kwa jina la "KITU BOMBA" itakuwa kitaani kesho. Akithibitisha hilo kwa njia ya simu mtoto wa King Majuto na ambae ndio meneja wake, Hamza Majuto amesema kuwa filamu hiyo itakuwa ikisambazwa na kampuni ya Steps duniani kote.


Hili ndilo kava la filamu hiyo mbele na nyuma

Pia jioni hii Hamza Majuto aliandika katika ukurasa wake wa face book kuwa watu wakae mkao wa kula kwani kazi imeshapikwa, ikapikika na kuiva hivyo basi wananchi pamoja na mashabiki wa filamu za vichekesho wasubiri burudani tu.


King Majuto

Hata hivyo juhudi za Makusudi za kumpata King Majuto ili azungumze japo machache kuhusu ujuio wa filamu hiyo ziligonga mwamba kutokana na kuwa ametingwa na shughuli nyingi za kujenga taifa.



Wednesday, January 30, 2013

KITALE ATANGAZA NDOA



Hamisi Kitale kwenye pozi la kazi

Msanii maarufu wa filamu za vichekesho Afrika Mashariki "kitale" ambaye amepata umaarufu sana kwa "style" yake ya uteja hivi karibuni amevunja ukimya na kufunguka kuwa  anatarajia kufunga ndoa siku ya jumapili ijayo. Akiongea na washkaji zake wa karibu kitale alisema katika maisha yake amepitia matatizo mengi na amekutana na changamoto za aina mbalimbali. Hivyo ameamua kuoa na kutulia kujenga familia iliyo bora. The Dj Max Entertainments tunampongeza na kumuombea kila la heri katika ndoa yake

Wednesday, January 23, 2013

SERENA WILLIAMS ATOLEWA JASHO NA CHIPUKIZI WA MIAKA 19

HUSSEIN MACHOZI: "NILITAMANI KUWA MCHEZAJI MAARUFU LAKINI MAISHA YAMENIFANYA NIWE MWANAMUZIKI MAARUFU"



Mwanamuziki maarufu wa "Bongo fleva" leo hii amefunguka alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha Leo tena cha Clouds fm. Akielezea historia ya maisha yake na shida alizokutana nazo mpaka kufikia hapo alipo leo hii, hadi kufanya jina lake halisi la Hussein Rashid kubadilika na kuwa "HUSSEIN MACHOZI"

Akielezea ndoto zake za kucheza timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania pia alifunguka kwa kusema kuwa kocha msaidizi wa sasa wa timu ya taifa (Jina kapuni) ndiye aliyevunja ndoto zake za kuendeleza kipaji chake cha mpira wa miguu wakati akiwa timu ya Kagera Sugar. Miongoni mwa vitu alivyokuwa akifanyiwa na kocha huyo na kumkatisha tamaa ni kupewa nguo za kocha huyo ali amfulie wakati wachezaji wengine wakiendelea na mazoezi.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa bado anaupenda sana mchezo wa mpira wa miguu kuliko muziki lakini hali ya maisha kwa sasa hamruhusu, labda kama atapata timu ambayo itamlipa vizuri.

NEW MUSIC VIDEO: KEISHA ft DIAMOND "NIMECHOKA"