Thursday, January 31, 2013

FILAMU YA MWISHO ALIYOCHEZA SHARO MILLIONEA KUWA MITAANI KESHOHussein "Sharo Milionea" enzi za uhai wake

Taarifa za kuaminika kutoka kwa familia ya "King Majuto" pamoja na Sharo zimetufikia hivi punde kuthibitisha kuwa ile filamu ya vichekesho aliyocheza Sharo siku chache kabla ya kukumbwa na umauti ambayo inajulikana kwa jina la "KITU BOMBA" itakuwa kitaani kesho. Akithibitisha hilo kwa njia ya simu mtoto wa King Majuto na ambae ndio meneja wake, Hamza Majuto amesema kuwa filamu hiyo itakuwa ikisambazwa na kampuni ya Steps duniani kote.


Hili ndilo kava la filamu hiyo mbele na nyuma

Pia jioni hii Hamza Majuto aliandika katika ukurasa wake wa face book kuwa watu wakae mkao wa kula kwani kazi imeshapikwa, ikapikika na kuiva hivyo basi wananchi pamoja na mashabiki wa filamu za vichekesho wasubiri burudani tu.


King Majuto

Hata hivyo juhudi za Makusudi za kumpata King Majuto ili azungumze japo machache kuhusu ujuio wa filamu hiyo ziligonga mwamba kutokana na kuwa ametingwa na shughuli nyingi za kujenga taifa.No comments:

Post a Comment