Thursday, October 11, 2012

KITENDO CHA DIAMOND KUVUA NGUO ON THE STAGE,... NINI TAFSIRI YAKO???



Gumzo lililopo kwa wadau wengi wa burudani ni kwa sasa ni juu ya kitendo cha msanii wa Bongo Fleva ambaye anashika chati ya juu kwa sasa "Diamond Platnumz" Nassib Abdul kushusha suruali yake mpaka chini na kubaki na nguo ya ndani kisha kuwapa mashabiki mgongo na kuinama.

Habari hii yazungumziwa sana kutokana na baadhi ya wasanii wa Bongo movi kukutwa na matukio kama hayo katika kipindi cha hivi karibuni na kukemewa vikali sana na baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya (bongo fleva). Jumamosi iliyopita katika kilele cha Tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam baadhi ya mashabiki hawakuamini macho yao baada ya msanii Diamond kufanya kituko hicho.

Kila mtu kwa upande wake anazungumzia tofauti kituko hicho, kuna gazeti lilidiriki kuandika eti kuwa amemuiga mpenzi wake wa zamani "Wema sepetu" kwani naye pia aliwahi kupatwa na mkasa kama huo kwa kuonesha baadhi ya sehemu za makalio yake kwenye jukwaa la Fiesta mwka jana. Pia kuna waliosema kuwa labda anamuiga afande sele kwani pia aliwahi kufanya kituko kama hicho miaka kadhaa iliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Na kuna mdau aliyeandika kwenye ukurasa wake wa face book " ah Diamond kama 50 cent"

JE WEWE MDAU TAFSIRI YAKO NINI???


No comments:

Post a Comment