Friday, October 5, 2012

MASIKINI LULU!!!! ARUDISHWA TENA LUPANGO NA KESI YAKE YAANZA UPYA
Elizabeth Michael (LULU)

Akiwa chini ya ulizi wa jeshi la polisi na kuhifadhiwa rumande kwa miezi kadhaa kutokana na tuhuma zinazomkabili za kusababisha kifo cha msanii mwenzie Steven Charles Kanuma. Msanii "lulu" leo alijikuta katika wakati mgumu baada ya mahakama ya rufaa kuamua kuwa kesi yake irudishwe mahakama ya kisutu na kuanza kusikilizwa upya kutokana na kutofuatwa kwa baadhi ya taratibu, ambapo Naibu msajili wa mahakama ya rufaa Bi Zahra Marume alitoa ufafanuzi huo masaa machache yaliyopita wakati kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa na kushindikana. 

No comments:

Post a Comment