Monday, July 30, 2012

TUPO SUZAME FESTIVAL YAFANA!!! MUANDAAJI BWANA ERIC MORO AWASHUKURU WOTE WALIOHUDHURIA KWA NIABA YA UONGOZI

WAKALI WA KUTOKA MOMBASA (SAV CLAN) WAACHIA SONGI JIPYA WAKIMSHIRIKISHA MH TEMBA NA DOGO ASLAY



 
Vijana wawili machachari kutoka Mombasa Kenya, Amour na Shirko ambao kwa pamoja wanaunda kundi la Sav Clan. Hapa wakiwa wamemshirikisha Dogo Aslay na mheshimiwa Temba ambao ni wakali kutoka Temeke Tanzania. Jina la ngoma ni "KICHECHE"

Sunday, July 29, 2012

JOSE CHAMELEONE AINGIA CHOO CHA KIKE





Huu ni msemo wa watoto wa mjini ikimaanisha kwamba mtu amejiingiza mtegoni au amejikuta yupo mahala asipotaka kuwa kwa wakati ule. Hapa tunafananisha kitendo cha msanii Jose Chameleone kutoka Uganda kuingia kwenye bifu na bwana Eric Shigongo, ni sawa na kuingia choo cha kike.

Eric James shigongo ni mwandishi maarufu wa vitabu Afrika Mashariki pia ni mmiliki wa kampuni ya Global Publishers ambayo inachapisha magazeti, ya Ijumaa, Amani, Uwazi, Champion pamoja na mengineyo nisiyoyajua mimi. Wachambuzi wa  mambo wanaweka swali bayana je magazeti ya Shigongo yatakuwa yakiandika nini kuhusu msanii Chameleone??? na sote tunatambua nguvu ya vyombo vya habari.

kwa niaba ya The Dj Max Entertainments tunakilani kwa nguvu zote kitendo cha utapeli kilichofanywa na msanii Jose Chameleone na wngineo wenye tabia kama yake tunawalaani pia. Kwani wasanii wa Afrika Mashariki wengi wamekuwa wakijiingiza katika utapeli wa namna hii na tutawafichua mmoja baada ya mwingine.

Saturday, July 28, 2012

JOSE CHAMELEONE NI TAPELI??? YASEMEKANA KUWA ANAFANYA KAZI ZAKE KWA UBABAISHAJI SANA!!!




AMEWAHI KUMPIGA CHANGA LA MACHO DJ JAY DEE

Dj Jaydee (Johhn Dillinga Matjor) muandaaji wa matamasha nchini Tanzania ambae pia aliwahi kufanyiwa utapeli na msanii Jose Chameleone mwaka 2005.

Sakata la msanii Jose Chameleone kutoka Uganda kuchuliwa hati yake ya kusafiria "Passport" na muandaaji wa matamasha ambae pia ni mmiliki wa kampuni ya Global Publisher, "the big name" Eric James shigongo lachukua taswira mpya. Ni baada ya mashuhuda lukuki kujitokeza na kutoa ushuhuda wao juu ya vitendo vya kihuni walivyofanyiwa na msanii huyo. 

Moja wa mashuhuda hao ni mtabgazaji wa radio na Dj maarufu nchini Tanzania mwenye asili ya South Africa Dj Jaydee, ambaye pia ni muandaaji wa matamasha.Dj Jaydee alitoa ushuhuda wake mbele ya waandishi wa habari hapo jana jijini Dar es Salaam.

ERIC SHIGONGO NAE AFUNGUKA KUHUSU "SKENDO" YAKE NA MSANII JOSE CHAMELEONE

Friday, July 27, 2012

HIVI NDIVYO CHAMELEONE ALIVYOOMBA MSADA WA KUPEWA PASSPORT YAKE NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA




Kitendo cha msanii Jose Chameleone wa Uganda kuchukuliwa Passport wake na muandaaji maarufu wa matamasha nchini Tnzania bwana Eric Shigongo chazua maswali mengi na mijadala. Je? wasanii wetu wa Afrika Mashariki wamekuwa matapeli? hawaridhiki na kipato chao? ni roho mbaya tamaa au wivu?

Inasemekana Chameleone kashawahi kufanya mambo kama hayo nchini Holland mpaka akashikiwa bunduki na muandaaji wa tamasha ndipo akapanda jukwaani. Pia aliwahi kufanya hivyo Belgium mwaka 2007, alipochukuwa hela za show na kuingia mitini. Na hivi sasa tayari kashachukua "advance" ya show kibao za majuu ambapo mojawapo inatarajiwa kufanyika Belgium jumamosi ijayo. Je atakuja????

MSANII JOSE CHAMELEONE ATOA UFAFANUZI KUHUSU SAKATA LAKE LA KUCHUKULIWA PASSPORT YAKE NA ERIC SHIGONGO