Friday, July 27, 2012

HIVI NDIVYO CHAMELEONE ALIVYOOMBA MSADA WA KUPEWA PASSPORT YAKE NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA




Kitendo cha msanii Jose Chameleone wa Uganda kuchukuliwa Passport wake na muandaaji maarufu wa matamasha nchini Tnzania bwana Eric Shigongo chazua maswali mengi na mijadala. Je? wasanii wetu wa Afrika Mashariki wamekuwa matapeli? hawaridhiki na kipato chao? ni roho mbaya tamaa au wivu?

Inasemekana Chameleone kashawahi kufanya mambo kama hayo nchini Holland mpaka akashikiwa bunduki na muandaaji wa tamasha ndipo akapanda jukwaani. Pia aliwahi kufanya hivyo Belgium mwaka 2007, alipochukuwa hela za show na kuingia mitini. Na hivi sasa tayari kashachukua "advance" ya show kibao za majuu ambapo mojawapo inatarajiwa kufanyika Belgium jumamosi ijayo. Je atakuja????

No comments:

Post a Comment