Sunday, July 29, 2012

JOSE CHAMELEONE AINGIA CHOO CHA KIKE





Huu ni msemo wa watoto wa mjini ikimaanisha kwamba mtu amejiingiza mtegoni au amejikuta yupo mahala asipotaka kuwa kwa wakati ule. Hapa tunafananisha kitendo cha msanii Jose Chameleone kutoka Uganda kuingia kwenye bifu na bwana Eric Shigongo, ni sawa na kuingia choo cha kike.

Eric James shigongo ni mwandishi maarufu wa vitabu Afrika Mashariki pia ni mmiliki wa kampuni ya Global Publishers ambayo inachapisha magazeti, ya Ijumaa, Amani, Uwazi, Champion pamoja na mengineyo nisiyoyajua mimi. Wachambuzi wa  mambo wanaweka swali bayana je magazeti ya Shigongo yatakuwa yakiandika nini kuhusu msanii Chameleone??? na sote tunatambua nguvu ya vyombo vya habari.

kwa niaba ya The Dj Max Entertainments tunakilani kwa nguvu zote kitendo cha utapeli kilichofanywa na msanii Jose Chameleone na wngineo wenye tabia kama yake tunawalaani pia. Kwani wasanii wa Afrika Mashariki wengi wamekuwa wakijiingiza katika utapeli wa namna hii na tutawafichua mmoja baada ya mwingine.

No comments:

Post a Comment