Thursday, March 21, 2013

"NEEMA WA MITEGO" NDIO JINA LA NGOMA MPYA YA NIKI MBISHI


Mbishi na Pozi la nguvu

Msanii wa muziki wa kufokafoka (HipHop) pande za Bongo mwenye jina kubwa kutokana na ubishi wake katika fani "Niki Mbishi" amefunguka na kusema ngoma yake mpya inatoka hivi karibuni ambayo itakwenda kwa jina la Ney wa mitego. Mbishi alifunguka na kusema kuwa ngoma hyo haina mahusiano yoyote na msanii Ney Wamitego na wala hajamzungumzia bali inamuhusu mwanadada Neema wa mitego ambaye kifupi chake ni Ney.

Mbishi amewataka mashabiki wake na mashabiki wa muziki kukaa mkao wakula na kusikiliya maisha halafu wao ndo watakuwa waamuzi. Aliendelea kusisitiza kuwa hiyo ngoma inamuhusu mwanadada Neema wa Mitego.

No comments:

Post a Comment