Thursday, May 31, 2012

MATUKIO MAWILI KWA MPIGO NDANI YA JIJI LA MUNICH JUMAMOSI HII



WAPENDA BURUDANI KAZI KWENU



Ikiwa zimesalia siku zipatazo mbili kufikia siku ya Jumamosi ya tarehe 2 mwezi june, wakazi wa jiji la Munich pamoja na maeneo ya jirani wanatarajia kupata burudani mbili za aina yake.


Mambo bado sound wakiwa wameshirikiana na malumbosjr.blogspot.de, wameandaa party ndani ya ukumbi wa Swing uliopo Maeneo ya Harras (Am Harras 2) huku muziki ukiporomoshwa na Dj Rama kwa kushirikiana na Dj Dully boy.


wakati huohuo The Mikocheni wakiwa wameandaa burudani kwa kuwaletea Party ya nguvu pia katika siku hiyihiyo (WHITE PARTY) ambayo itakuwa ikitokea pale maeneo ya Ostbahnhof katika ukumbi wa Storchenburg (Friedenstraße 10). Bila ya kusahau muziki kutoka kwa Dj Sidekickz akishirikiana na Dj Tindo.

                      WAPENDA BURUDANI KAZI KWENU

No comments:

Post a Comment