Thursday, November 1, 2012

DAVID ALABA KUFUNGUA KESI DHIDI YA KITUO CHA T.V CHA "ORF" KWA KUMDHALILISHAMchezaji kinda ndani ya nyota nyekundu ya kusini "FC BAYERN" raia wa Austria mwenye asili ya mchangiko wa kiafrika na Asia (baba kutoka Nigeria na mama kutoka Ufilipino). David Alaba amepeleka malalamiko kwa mwanasheria wake na kutaka kufungua kesi dhidi ya kituo hicho cha nchini Austria kwa kitendo ambacho alikiona ni cha kudhalilisha na kumbagua. Kupitia kipindi chake cha Commedy, walimuonyesha mtu mweusi mwenye jezi ya Bayern akiwa na tajiri wa kizungu kutoka Canada.

Matukio yaliyomkera Alaba ni pamoja la tajiri huyo kumuonyesha ndizi (chakula cha nyani) Alaba, pia kumuuliza kama anaishi kwenye nyumba za ukimbizi au nyumba za mabati zilizoezekwa na nyasi. Pia mtu huyo alimuuliza Alaba kama ana elimu au amewahi kwenda shule kwa kuwa "Black man" anawaza hela tu. Hata hivyo kituo hicho cha TV kiliomba radhi kwa mchezaji huyo na kuweka wazi kuwa hawakuwa na lengo la kumdhalilisha. Mpaka sasa Alaba hajaonyesha bado dhamira yoyote ya kubadili msimamo wake juu wa kufungua kesi dhidi ya televisheni hiyoNo comments:

Post a Comment