Friday, November 30, 2012

KITALE AWALAANI WALIOMFANYIA UBAYA SHARO MILIONEA



Swahiba wa karibu wa marehemu "Sharo" na pia ni mshirika wake mkubwa kwenye kazi za muziki na sanaa ya uchekeshaji "Kitale" Juzi alilaani vikali na kuwalaani waliomfanyia vitendo visivyo vya kibinaadam Sharo baada ya kupata ajali. Kitale aliongea kwa masikitiko na uchungu mkubwa alipokuwa akihojiwa na Millard Ayo wa Clouds Fm, "Watanzania hawana huruma, wamemvua marehemu mpaka viatu yani wamemuacha na nguo ya ndani tu" hayo ni baadhi ya maneno aliyoyasema Kitale.

Kiukweli kabisa kitendo hicho hakina hata chembe ya uungwana hasa ukizingatia ajali mbaya kama hiyo aliyoipata Sharo, watu badala ya kufika eneo la tukio nakutoa msaada badala yake wanaenda kufanya vitendo vya wizi na uhalifu. Pia kitale alisema kuwa marehemu wakati anaondoka alikuwa na jumla ya shilingi za kitanzania milioni 6 ambazo pia hazikupatikana. Huku akiwa na sura iliyojaa machungu kitale aliongea maneno hayo kwa huzuni alihani kana kwamba haamini kama ni kweli kampoteza swahiba wake.

Kwa niaba ya " THE DJ MAX ENTERTAINMENTS" tunaungana na kitale na waungwana wengine wote kulaani kitendo kisicho cha kibinadamu alichofanyiwa marehemu "Sharo".Pia tunalaani matendo kama hayo katika ajali nyinginezo. Vilevile tunatoa pole kwa Familia ya wafiwa, ndugu jamaa na Marafiki. Mungu ailaze pema roho ya Marehemu. Ameen!

No comments:

Post a Comment