Friday, July 20, 2012

AMIRI KOBA MATIGA, MWANABAGAMOYO ALIYEPANIA KUIVUMISHA SAUTI YA NGOMA DUNIA NZIMA

Tunapoizungumzia sanaa ya ngoma za asili na Sarakasi basi hatutomaliza kauli zetu bila ya kuhusisha jina Matiga. Ambaye ni kijana mdogo mwenye asili ya Bagamoyo na mzaliwa wa wilaya ya Bagamoyo mkoani pwani. Amekuwa akitangaza utamaduni wa Tanzania kwa juhudi zake binafsi nje ya mipaka ya tanzania. 

Pia aliwahi kushiriki katika "program" maalum ya mabadilishano ya vijana ya kitamaduni kati ya Tanzania na Norway. Mradi huo ujulikanao kama SPOR nchini tanzania unasimamiwa na Flame Tree Media Trust chini ya uongozi wa bwana Mwanzo Laurent Milinga 

Matiga (aliyekaa chini mbele) akiwa na washirika wake baada ya onyesho nchini Marekani wakiwa katika pozi la picha ya Pamoja.

Pamoja na kuishi kwa Obama lakini matiga bado anaendeleza sanaa yake kwa hali na mali na hivi karibuni anatarajia kufanya ziara kubwa sana barani ulaya
Mtoto wa Bagamoyo akiwa jukwaani anaonyesha manjonjo yake katika moja ya maonyesho yake
Pamoja na kuishi majuu lakini Matiga bado anaishi maisha yake halisi aliyokulia ya kitamaduni, hapa alikuwa anapika chapata badala ya kujichanganya kwenye migawaha ya kifahari.

No comments:

Post a Comment