Monday, July 23, 2012

TUPO PAMOJA FESTIVAL IN NÜRNBERG



Ni tamasha la kujitolea (none-profit) ambalo limeandaliwa na kijana mtanzania anayeishi katika mji wa Nürnberg nchini ujerumani, na linatarajiwa kufanyika siku ya jumapili ya tarehe 29 mwezi huu. Lengo la tamasha hili ni kukusanya michango kwa ajili ya kuendeleza kituo cha watoto waliotokea katika mazingira magumu na wenye vipaji. Kikubwa zaidi kinachofanyika ni kukuza na kuendeleza vipaji vyao ili waweze kujiajiri wenyewe katika maisha yao ya baadae.


Vilevile tamasha hili litakuwa ni sehemu ya kukusanya michango kwa ajili ya kuwafanya walimu na walezi wa watoto hao waweze kujikimu kimaisha. Ikumbukwe pia vifaa vya michezo kama mipira, viatu na jezi ambazo zipo katika hali nzuri zinapokelewa kwa ajili ya kuzituma Tanzania kusaidia watoto hao. Bila ya kusahau vifaa vya muziki kwa mfano magitaa, vinanda na kadhalika pia vinapokelewa wakati wowote hata baada ya tamasha.



Mratibu wa shughuli nzima bwana Eric ambae anafanya kazi hii kwa kujitolea akiwa katika moja ya hafla alizowahi kuziandaa katika kukusanya michango ya kusaidia kuinua vipaji vya watoto.


(Ratiba ya shughuli nzima)

Tamasha hili linatarajiwa kuanza majira ya saa saba mchana siku ya jumapili ya tare 29-07-2012 ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa ujerumani na wengine kutoka nje ya ujerumani.

Shughuli nzima itakamilishwa na burudani ya muziki kutoka kwa Dj Mukada kutoka Tanzania.Pia kutakuwa na maonyesho ya mavazi na mafunzo maalum ya kupiga ngoma kwa watoto na wakubwa.


(Dj Max akicharaza Ngoma)

Badala ya kupiga muziki wa mashine kama ilivyozoeleka siku hiyo Dj Max atarudi katika asili yake na kucharaza ngoma za asili na kuuthibitishia umma kuwa yeye ni Mzaramu halisi wa Bagamoyo. usikubali kuhadithiwa, njoo ujionee mwenyewe.


KIINGILIO NI BURE,  NYOTE KARIBUNI!!!

No comments:

Post a Comment