Thursday, July 26, 2012

ARBA WA KUKAYE MOTO BAND KUWASHA MOTO NDANI YA TUPO PAMOJA FESTIVAL IN NÜRNBERG JUMAPILI HII





Kazi ya ubunifu ikionyesha jinsi ratiba ya shughuli nzima itakavyokuwa, ambapo mwanamuzi maarafu wa kitanzania anaeishi Ujerumani kutoka kwenye kundi la Kukaye Moto pia ataonyesha manjonjo yake.

 Ikumbukwe kuwa tamasha hili ni kwa ajili ya kukusanya vifaa vya michezo na muziki kwa ajili ya watoto waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu. Lengo ni kuendeleza vipaji vyao ili waweze kujitegemea baadae. Vilevile kukusanya michango kwa ajili ya walimu na walezi kuweza kujikimu kimaisha.




Muandaaji wa shughuli hiyo na pia mlezi wa watoto Bwana Eric Moro akiwa na wageni waliomtembelea katika banda lake kwenye maonyesho ya Tamasha la kiafrika (Afrcan Festival) Nürnberg mwezi "June" Mwaka huu.

Tamasha la kujitolea Nürnberg linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii 29-July-2012 siku ya jumapili kuanzia saa saba za mchana katika mji wa Nürberg nchini Ujerumani.

Nyote mnakaribishwa kwa kiingilio cha bure

No comments:

Post a Comment