Thursday, August 23, 2012

AFYA YA BI KIDUDE SI NZURI KWA SASA, AUGUZWA NA MJUKUU WAKE NYUMBANI KWAKE ZAZNZIBAR




Mwanamuzi mkongwe duniani bi kidude, amabae ni mzaliwa wa Zanzibar Tanzania kwa sasa yuko kitandani amabapo bado haijajulikana rasmi anasumbuliwa na maradhi gani (daktari hajathibitisha). Tangu alipoanza kutojisikia vizuri kwa zaidi ya wiki sasa yupo tu nyumbani kwake akiuguzwa na mjukuu wake.

Utafiti wa kitaalam wala msada wa kitaalam hajapatiwa pia hakuna mdau yoyote wa muziki kutoka nchini Tanzania wala bara la Afrika aliyefika kumjulia hali mpaka sasa, hayo aliyasema mjukuu wake wakati alipokuwa akitoa malalamiko yake kupitia sauti ya Tanzania Zanzibar.

Kwa niaba ya "The Dj Max Entertainments" tunamuomba Mungu amuondolee maradhi na amrudishie afya yake apate kuwa mzima na kuendeleza gurudumu la muziki kama kawaida. Mwenyezimungu atampa bibi yetu afueni "AMEEN"

No comments:

Post a Comment