Wednesday, August 15, 2012

UP COMING STAR "BOBBY ST" LIVE in MUNICH on 1st SEPTEMBER 2012

Msanii anaekuja juu kwa kasi mwenye asili ya Kenya ambae anaishi ujerumani, anatarajiwa kutoa burudani ya  aina yake kwenye tamasha kubwa la kihistoria (EAST vs WEST AFRICAN PARTY vol 2). Ambalo limeandaliwa na the Dj Max Entertainments kwa kushirikiana na Shounkemp Int. Studio Jay Musik.

Pia kutakuwa na burudani mbalimbali za muziki siku hiyo ambapo ma Dj wakali kutoka East an West Africa watakuwa wakionyesha uwezo wa kuchezea mashine.

Kutoka East safu ya muziki itaongozwa na Dj Rama, Dj Dully boy na mwanadada machachari Dj Lady Kiarie. Vilevile kama afya ya mkono itaendelea vizuri Dj Max nae atarejea ulingoni kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji wa mkono kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

Wakati upande wa West burudani itatolewa na Dj Korea, Dj Timberland bila kumsahau Dj Jay, kila mtu anakaribishwa kula bataNo comments:

Post a Comment