Thursday, August 23, 2012

MAY D APIGWA CHINI P SQUARE RECORDS




Tetesi zimezagaa kuwa kuna kutokuelewana kati ya uongozi wa P square records na msanii May D ambae pia ni kutoka Nigeria kitendo ambacho kimesababisha msanii huyo kuenguliwa kwenye lebo hiyo. Mwenyewe May D anasema hana taarifa hizo rasmi kutoka kwa uongozi wakati wadaku wa karibu wanasema msanii huyo hajawahi kufanya makubaliano ya kimaandishi na lebo hiyo, yalikuwa ni makubaliano ya kiushkaji tu kwa njia ya mdomo.

May D ni msanii kutoka Nigeria ambaye alimeremeta vizuri sana kwenye "vesi" ya pili ya wimbo wa "Chop my money remix" na kuonyesha uwezo wa hali ya juu aliposhirikishwa na mabosi zake hao wa P square

No comments:

Post a Comment