Thursday, August 23, 2012

BAADA YA KUCHEZEA KICHAPO KITAKATIFU "ZOLA D" ATOA SABABU LUKUKI




Sijui ni mila, utamaduni, desturi, kawaida au mazoe kwa wanamichezo wa Tanzania wanaposhindwa huwa hawakubali kama wameshindwa kihalali na badala yake kutoa vijisababu vya ajabu ajabu, hayo yalikuwa maneno yaliyotolewa na mmoja kati ya mashabiki waliohudhuria mpambano wa masumbwi kati ya Zola D ambaye pia ni mwanamuziki wa bongo fleva na Mchumia Tumbo.

Shabiki huyo alifyatuka maneno hayo baada ya kusikia maneno ya Zola akijitetea eti kuwa ulingo ulikuwa umelowa maji na ndio sababu ya yeye kuanguka wakati alipojaribu kumshambulia mpinzani wake. "Inamaana kama ulingo ulikuwa na maji, huyo mchumia tumbo alipigana na mtumbwi au boti?" aliendelea kuropoka shabiki huyo. Huku sauti kutoka kwa shabiki mwingine ikisikika akisema " basi na yeye Zola angepewa ngalawa" kisha wote wakacheka na kukata simu.

Hapo ndipo ukawa mwisho wa mahojiano yangu na wadau hao, kama una maoni unaweza kuyasogeza kupitia:  djmaxentertainments@yahoo.de


No comments:

Post a Comment