Tuesday, August 21, 2012

PROMOTA WA MAJUU NA PROMOTA WA BONGO USO KWA USO




Muandaa matamasha maarufu barani Ulaya mtanzania anaeishi Norway Hassan Nganzo ambaye pia anafahamika kwa jina la kaka mkubwa, ikiwa ni heshima anayopewa na wadau wa muziki na burudani barani Ulaya (mwenye shati jeupe wa kwanza kushoto) Juzi kati mnamo wiki ya mwisho ya mfungo alipata wakati wa kupiga story na Saidi Fella (mwenye fulana ya blue, wakwanza kulia) katika hafla ya futuru iliyoandaliwa na kundi la Tiptop connection la Manzese Dar.

Baada ya kalamu hiyo ambayo pia iliwakutanisha Abdul bonge na Babu Talle (mwenye fulana nyekundu) wadau hao wa muziki wa kizazi kipya walipata muda wa kujadiliana mawili matatu juu ya changamoto zinazowakabili waandaji wa matamasha Afrika na Ulaya ikiwa sasa kuna vuguvugu la baadhi ya wasanii kujihusisha na vitendo vya kitapeli, hasa wasanii wa bongo fleva.

Hassan Nganzo (kaka mkubwa) yupo Tanzania sasa kwa ziara ya kikazi na mapumziko mafupi, tunamtakia kila la heri na pia atuwakilishe vyema wadau wa muziki wa kizazi kipya barani Ulaya

No comments:

Post a Comment