Saturday, September 22, 2012

DAVID ALABA APATA NAFUU
Lile jembe la ukweli kutoka kijiji cha vipaji maeneo ya Säbenerstr jijini Munich, makao makuu ya chama kubwa Fc Bayern. Kijana mwenye umri mdogo kuliko wote katika kikosi cha kwanza David Alaba ameanza kupata nafuu kutokana na majiraha aliyoyapata kwa zaidi ya mwezi sasa.

Alaba aliwadhihirishia mashabiki kuwa anaendelea vizuri pale alipoingia mazoezini asubuhi ya leo na kupasha misuli kwa kukimbia hapa na pale huku akiwasalimia mashabiki waliohudhuria mazoezini hapo.

No comments:

Post a Comment