Tuesday, September 18, 2012

NGOMA AFRIKA BAND WAACHA GUMZO BREMEN


Ras Makunja na vijana wake wakiwasha moto

Ni kundi la muziki wa dansi linaloundwa na vijana wa ki Tanzania kwa kushirikiana na vijana wenzao kutoka Congo ambapo wote kwa pamoja wanaishi nchini ujerumani. Chini ya uongozi wa Captain Ras Makunja (mtanzania) juzi waliacha wakizungumziwa baada ya kutoa show ya nguvu katika mji wa Bremen nchini ujerumani. Kwa hakika walikonga nyoyo za mashabiki wariohudhuria na pia kuwakumbusha nyumbani wazungumzaji wa lugha ya kiswahili pale walipoimba nyimbo za kiswahili. Yani ilikuwa ni burudani ya aina yake.Baadhi ya masahbiki waliohudhuria wakiserebuka na kujimwaga uwanjani kuburudika na burudani tamu ya Ngoma Afrika Band


No comments:

Post a Comment