Tuesday, September 25, 2012

OLIC NA MANDZUKIC WALIJITABIRIA KUWA WATABADILISHANA TIMU???Mara ya mwisho walipokutaka katika uwanja wa Allianz Arena msimu uliopita wa ligi ya Ujerumani (Bundesliga). Wachezaji Mario Mandzukic na Ivica Olic walikuwa wakichezea timu mbili tofauti na wanazocheza sasa. Ambapo Olic alikuwa Fc Bayern Munich na sasa amehamia Wolfsburg, na Mandzukic alikuwa VfL Wolfsburg na sasa amehamia Bayern. Jioni ya leo wawili hao wanatarajia kukutana tena kwenye uwanja wa Allianz Arena kwa mara nyingine wakiwa wamebadilishana timu. 

Wachunguzi wa mambo wanajiuliza je, walipobadilishana jezi katika msimu uliopita ni kama walikuwa wakitabiri kuwa watabadilishana timu baada ya msimu wa ligi kuisha? au kila mmoja alikuwa anaitamani timu ya mwenzie? kwa maana Olic alikuwa anatamani kuchezea Wolfsburg na Mndzukic alitamani kucheza Bayern???


No comments:

Post a Comment